15th February 2017 15:45:14

TAARIFA KWA VYUO/TAASISI KUHUSU UTOAJI WA MATANGAZO KWA UMMA JUU YA PROGRAMU ZA MAFUNZO ZINAZOTOLEWA

 

 

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI

(NACTE)

 

 

TAARIFA KWA VYUO/TAASISI KUHUSU UTOAJI WA MATANGAZO KWA UMMA JUU YA PROGRAMU ZA MAFUNZO ZINAZOTOLEWA

 

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa sheria ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Sura ya 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi nchini. Sheria hii inavitaka Vyuo/Taasisi zote zinazotoa elimu ya ufundi kusajiliwa kabla ya kuanza kuendesha mafunzo yoyote. Aidha, Baraza huidhinisha mitaala kabla haijaanza kutumika.

  

Kumekuwepo na tabia kwa baadhi ya Vyuo/Taasisi kutoa matangazo kwa umma kuhusu programu ambazo hazijaruhusiwa na Baraza kutolewa kwenye Chuo/Taasisi husika, au kutangaza sifa pungufu/hafifu za kujiunga na programu hizo. Matangazo haya yanapotosha umma kuhusu sifa stahiki za kujiunga na programu hizo.

  

Kwa Waraka huu, Baraza linaelekeza Vyuo/Taasisi kutoa Matangazo kwa mujibu wa Kitabu cha Mwongozo wa Udahili (Admission Guidebook) wa Mafunzo yanayotolewa na Vyuo/Taasisi zilizosajiliwa na Baraza (bonyeza hapa kuona Kitabu cha Mwongozo wa Udahili).

  

Aidha,Vyuo/Taasisi zitakazotoa Matangazo yanayopotosha umma zitachukuliwa hatua za Kisheria ikiwemo kufungiwa kutoa Mafunzo.

  

IMETOLEWA NA:

OFISI YA KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)