22nd July 2017 17:10:05

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2017 WANAOKUSUDIA KUOMBA KUJIENDELEZA KATIKA NGAZI YA CHETI AU STASHAHADA KATIKA VYUO VINAVYOSIMAMIWA NA BARAZA KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2017 WANAOKUSUDIA KUOMBA KUJIENDELEZA KATIKA NGAZI YA CHETI AU STASHAHADA  KATIKA VYUO VINAVYOSIMAMIWA NA BARAZA  KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018

Baraza linapenda kuwataarifu wahitimu wa kidato cha sita waliohitimu mwezi Mei, 2017 na umma kwa ujumla; kuwa sasa wanaweza kutuma maombi  ya Udahili wa kozi za Afya na Ualimu katika Vyuo vya Serikali  kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz) au kupitia vyuo husika vya Afya na Ualimu ambavyo vitashughulikia maombi hayo na kufanya Udahili kwa njia ya mtandao kupitia ‘Institutional Panel’ zao.

Kwa wale ambao walishatuma maombi na wanataka kuongeza sifa ya kidato cha sita wanaweza kufanya hivyo sasa kupitia kurasa zao binafisi (Profile).Pia baraza linapenda kuwakumbusha na kuwahimiza wote wenye sifa kama zilivyo ainishwa kwenye kitabu cha Muongozo wa Udahili (Admission Guidebook) kinachopatikana kwenye tovuti ya Baraza kuwa, wafanye maombi yao mapema kabla ya tarehe 20 Agosti, 2017 kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza kwa sababu hakutakuwa na muda wa nyongeza.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

TAREHE: 22/07/2017