Admissions to Degree Courses for 2012/13 (Swahili)
UTANGULIZI
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (‘Tanzania Commission for Universities’-TCU) ikishirikiana na
Baraza laTaifa la Elimu ya Ufundi (‘National Council for Technical Education’ - NACTE) pamoja
na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi Elimu ya Juu (Higher Education Students Loans Board)
inapenda kuutarifu umma kuhusu utaratibu wa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu kwa mwaka
wa masomo 2012/2013 kupitia mfifumo ya “Pre-entry”, “Mature Age Entry”, “Equivalent
Qualifications” na mfumo wa pamoja wa udahili (‘Central Admission System’) na utaratibu wa
mikopo kama ifuatavyo:
1. MFUMO WA UDAHILI KUANZIA MWAKA 2012/13
1.1 Utaratibu wa Kuendesha Program za “Pre-entry” na “Mature Age Entry”
Kuanzia mwaka huu 2012, vyuo vyote vitakavyotaka kuendesha mafunzo ya awali kabla ya
mwombaji kustahili kudahiliwa ili kuweza kujiunga na programu za elimu ya juu (pre-entry
programmes) pamoja na kuendesha mitihani ya kupitia mfumo wa “Mature Age Entry”
vinatakiwa kuwasilisha programu hizo Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) au Baraza la Taifa la Elimu ya
Ufundi (NACTE) kwa uhakiki na kupata kibali. Programu hizo ni lazima ziendeshwe kwa muda
wa mwaka mmoja. Hali kadhalika kwa upande wa mitihani kupitia mfumo wa mature entry,
Tume kwa ushirikiano na Baraza, kwa pamoja wataandaa na kuratibu utaratibu wa mitihani
katika vituo maalum kikanda ili Vyeti vitakavyotolewa viwe na ulinganifu unaostahili na
hatimaye kuweza kutumika katika udahili wa sifa linganishi katika vyuo mbalimbali.
Vyuo vinatakiwa kuandaa programu za mifumo ya “pre-entry” na “Mature age entry” na
kuziwasilisha Tume na Baraza ili zihakikiwe kwani mwaka wa masomo kwa kusudi hili utaanza
mwezi Agosti 2012/2013. Kwa utaratibu huu, watakaofanya mafunzo hayo watatakiwa kufanya
mitihani yao na kujiunga na masomo ya elimu ya juu katika mwaka wa masomo 2013/2014.
Kwa taarifa hii, mwaka 2012/13 hakutakuwapo na udahili wa wanafunzi kwa mfumo wa “Pre-
Entry” na “Mature Age Entry”.
Zaidi download attachment usome.
film izle oriflame üyelik film izle - youtube - celal ile ceren - celal ile ceren izle - celal ile ceren full izle - h˝zl˝ ve ˆfkeli 6 full izle - h˝zl˝ ve ˆfkeli 6 izle - CM101MMXI Fundamentals Full izle - Romantik Komedi 2 Bekarl˝a Veda izle - Romantik Komedi 2 Bekarl˝a Veda Full izle - kelebein r¸yas˝ - kelebein r¸yas˝ izle - kelebein r¸yas˝ full izle - Mutlu aile defteri izle - Mutlu aile defteri full izle
To read the news clip click (

31.4 Kb)