TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAOMBI YA NAMBA YA UHAKIKI WA TUZO (AVN)

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAOMBI YA 
NAMBA YA UHAKIKI WA TUZO (AVN)

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura ya 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi katika Vyuo  vinavyotoa mafunzo kwa ngazi za Astashahada, Stashahada na Shahada ambavyo si Vyuo Vikuu au Vyuo Vikuu Vishiriki nchini.

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi linapenda kuwafahamisha wahitimu wa Stashahada wanaotaka kujiendelezana Elimu ya Juu kwamba Baraza linaendelea kutoa Namba za Uhakiki wa Tuzo (Award Verification Number – AVN). 

Baraza linapenda kuufahamisha umma kwamba kwa Vyuo vyote vilivyowasilisha taarifa za wahitimu hao tayari zote zimefanyiwa kazi na wahitimu wanaweza kuendelea kutuma maombi ya AVN sasa.

Maombi yanayopokelewa yanafanyiwa kazi ndani ya muda mfupi na kupatiwa AVN.

Aidha Baraza linatoa ilani kwa Vyuo vyote ambavyo havijawasilisha taarifa za wahitimu (matokeo ya mitihani) ili waweze kupatiwa AVN kuhakikisha vinafanya hivyo kabla ya tarehe 31 Agosti, 2019 ili kuondoa usumbufu kwa waombaji.

Baraza litachukua hatua kali kwa Vyuo ambavyo vinachelewesha taarifa za wahitimu na hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa wahitimu hao na wananchi wote kwa ujumla bila sababu za msingi.

IMETOLEWA NA: 
OFISI YA KATIBUMTENDAJI
BARAZALA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAREHE: 26/08/2019