TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UDAHILI WA WANAFUNZI KATIKA VYUO VYA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI MKUPUO WA SEPTEMBA 2022/2023

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO YA UFUNDI  STADI (NACTVET)

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UDAHILI WA WANAFUNZI KATIKA VYUO VYA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI – MKUPUO WA SEPTEMBA 2022/2023

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linaujulisha umma kuwa dirisha la maombi ya udahili kwa awamuya pili kwa vyuo vya Afya na Sayansi Shirikishi limefungwa rasmi tarehe 30 Agosti, 2022. 

Hadi tarehe 30 Agosti, 2022, Baraza lilipokea jumla ya maombi ya awamu ya pili 8183 (wanawake 4132 (50.5%) na wanaume 4051(49.5%) kupitia Udahili wa Pamoja (Central Admission System CAS) katika Vyuo 174 vya Afya. Katika awamu hii ya pili, majibu ya waombaji watakaochaguliwa kujiunga na vyuo vyaAfya na Sayansi Shirikishi yatatolewa tarehe 6 Septemba, 2022.

Dirisha la awamu ya Tatu la Udahili wa Pamoja kwa kozi za Afya na Sayansi Shirikishi litafunguliwa kuanzia tarehe 8 mpaka tarehe 23 Septemba, 2022. Hivyo, waombaji ambao hawakupata nafasi katika dirisha la awamu ya Kwanza na la Pili, wanashauriwa kuomba tena katika dirisha la Tatu. 

Aidha, kwa waombaji wa kozi zisizo za Afya na Sayansi Shirikishi, vyuo vitaendelea kuwasilisha majina ya wanafunzi kupitia mfumo wa udahili wa Baraza kwa ajili ya uhakiki wa sifa hadi tarehe 2 Septemba, 2022. Majibu ya waombaji waliohakikiwa yatatoka tarehe 17 Septemba, 2022 kama inavyooneshwa kwenye Kalenda ya Matukio ya Baraza.

IMETOLEWA NA OFISI YA KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI

TAREHE 31 AGOSTI, 2022