TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UHAMISHO WA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA NA OR-TAMISEMI KUJIUNGA NA TAASISI YA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI DODOMA

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI (NACTVET)

This image has an empty alt attribute; its file name is NACTVET-logo.jpeg

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UHAMISHO WA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA NA OR-TAMISEMI KUJIUNGA NA TAASISI YA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI DODOMA KWENYE PROGRAMU YA UTABIBU KWA MWAKA WA MASOMO 2022/2023

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linapenda kuutarifu umma kwamba wanafunzi waliochaguliwa na OR-TAMISEMI kujiunga na Taasisi ya Afya na Sayansi Shirikishi Dodoma (Dodoma Institute of Health & Allied Science) kwenye programu ya Utabibu kwa mwaka wa masomo 2022/2023 wamehamishwa kwenda kujiunga na Chuo cha Afya na Teknolojia Singida (Singida College of Health and Technology). Sababu ya uhamisho huo ni kwamba chuo walichochaguliwa awali hakitatoa mafunzo hayo kwa mwaka huu.

Hivyo, wanafunzi wanatakiwa kuwasiliana na Chuo cha Afya na Teknolojia Singida ili kupata taratibu za kujiunga na chuo hicho kabla ya tarehe 3 Oktoba, 2022.

 

IMETOLEWA NA:

OFISI YA KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI (NACTVET)

19/09/2022