TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UDAHILI WA MKUPUO WA MACHI KWA MWAKA WA MASOMO 2023/2024

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI (NACTVET)

This image has an empty alt attribute; its file name is NACTVET-logo.jpeg

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UDAHILI WA MKUPUO WA MWEZI MACHI KWA MWAKA WA MASOMO 2023/2024

Baraza linautaarifu umma kwamba Udahili wa mkupuo wa mwezi Machi (March intake) kwa Mwaka wa Masomo 2023/2024 umeanza rasmi tarehe 16 Januari, 2023. Vyuo vinavyoruhusiwa kudahili wanafunzi katika mkupuo huu ni vyote vyenye uwezo, isipokuwa vyuo vinavyotoa mafunzo ya Afya na Sayansi Shirikishi kwa Tanzania Bara.

Vyuo vya Afya na Sayansi shirikishi vilivyopo Tanzania Visiwani vyenye uwezo wa kudahili katika mkupuo huo vinarushusiwa ikiwa vitakidhi vigezo.

Hivyo, Baraza linavielekeza vyuo vinavyohitaji kudahili wanafunzi kwa mkupuo huu kutuma maombi kabla ya tarehe 27 Januari, 2023 kwa kujaza fomu inayoonesha uwezo wa chuo kuendesha mafunzo na kuiwasilisha katika Ofisi za kanda za Baraza ambapo chuo kipo. Uwezo huo ni pamoja na kuwa na miundo mbinu na walimu wa kutosha kutoa mafunzo katika mikupuo miwili kwa mwaka (Machi na Septemba). Fomu ya maombi inapatikana katika tovuti ya Baraza www.nacte.go.tz  sehemu ya Downloads kwa kubofya fomu ya maombi ya udahili march intake 2023/2024.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI (NACTVET)
17/01/2023