Mkataba wa Huduma kwa Mteja

Utangulizi

Mkataba wa huduma kwa mteja ni ahadi ambayo Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linaweka kama mtoaji wa huduma kwa wateja wake. Mkataba huu unatoa viwango vya huduma zinazotolewa na Baraza. Pia unaainisha Haki na Majukumu ya Baraza na mteja katika utoaji na utumiaji wa huduma na jinsi mteja anavyoweza kupata huduma hizo.

Baraza linakusudia kutoa huduma zenye viwango vya ubora kama vilivyoainishwa katika mkataba huu ili kutimiza malengo yake. Malengo hayo ni pamoja na kuhakikisha kuwa wateja wanapata huduma bora katika uendeshaji wa elimu ya ufundi ; usajili na ithibati wa vyuo vya elimu ya ufundi , usajili wa walimu na udahili; na ulinganisho wa vyeti, uidhinishaji wa mitaala na uhakiki wa vyeti.

Aidha, Baraza linakusudia kutoa taarifa ya tathmini ya huduma inazozitoa kila mwaka kwa wateja na wadau wengine kama namna ya kuendelea kuinua ubora wa huduma kwa wateja wake.

Ili kwenda sambamba na kasi ya mabadiliko katika tasnia ya utoaji huduma na maendeleo ya elimu ya ufundi, Baraza litalazimika kufanya marekebisho ya mara kwa mara ya mkataba huu ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya maendeleo ya elimu ya ufundi.

Ni matarajio yetu kuwa mtashirikiana nasi kwa kutoa mrejesho kwa njia mbalimbali ili kutuwezesha kuwapa huduma bora zaidi na kukidhi matarajio yenu.
Tunawakaribisha wateja kutumia huduma zetu.

Kwa maelezo zaidi bofya hapa chini.

Mkataba wa Huduma kwa Mteja